Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania tatizo lipo hapa...

Polisi TZZ Kikosi cha Polisi Tanzania

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Polisi Tanzania ni kati ya timu zilizoanza Ligi Kuu Bara vibaya msimu huu hadi sasa imecheza mizunguko tisa ikiwa mkiani, imeshinda mechi moja pekee hadi sasa, sare mbili, vichapo sita na kukusanya pointi tano tu.

Polisi Tanzania ipo vibaya ukilinganisha na msimu uliopita mbao hadi mzunguko wa nne ilikuwa inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 12 huku ikiwa na kinara wa ufungaji katika ligi wakati huo Vitalis Mayanga aliyekuwa na mabao matano.

Kuna sababu nyingi zilizochangia timu hiyo kufanya vibaya katika michezo hiyo iliyocheza hadi sasa na Mwanaspoti linakuletea kati ya changamoto za timu hiyo hadi kufikia hapo ilipo sasa.

WACHEZAJI WALIOONDOKA

Kati ya sababu zilizochangia timu hiyo kufanya vibaya ni kuachana na wachezaji wake muhimu waliokuwa wakitumika katika kikosi cha kwanza kutokana na ubora wao.

Polisi Tanzania iliachana na wachezaji saba waliofanya vizuri msimu uliopita na kutimkia timu nyingine na wamekuwa msaada huko kutokana na ubora walioanza nao msimu huu.

Wachezaji hao ni Kassim Haruna ‘Tiote’ aliyetimkia Namungo, Baraka Deusdedit na Yahya Mbegu wote (Geita Gold), Said Juma Makapu (Ihefu), Metacha Mnata (Singida Big Stars) na Tariq Seif (Mbeya City).

Aidha, katika dirisha dogo msimu uliopita Polisi Tanzania iliachana na beki aliyekuwa muhimili wa timu katika kuzuia mashambulizi na kuanzisha mashambulizi ambaye pia ni mzoefu Kelvin Yondan aliyekwenda Geita Gold.

BENCHI LA UFUNDI

Changamoto nyingine Polisi Tanzania inakutana nayo ni upya wa benchi la ufundi. Msimu uliopita ilikuwa na kocha, Malale Hamsini ila msimu huu iliachana naye, akatimkia JKT Tanzania.

Uongozi wa Polisi Tanzania ulimpa kazi ya kukinoa kikosi hicho kocha, Joslin Sharif Bipfubusa, raia wa Burundi, aliyewahi kufundisha timu ya taifa ya Burundi, Rwanda, DR Congo ambaye naye ameondolewa kwenye benchi hilo.

Polisi Tanzania ina wachezaji wengi wapya ambao bado hawajazoea mazingira pamoja na kupata maelewano na wale waliokuwapo msimu uliopita hapo hapo anaingia kocha mpya.

Ugeni wa kocha na nyota wengi wapya vinaifanya timu kuwa inajengwa mpya na hapakuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi.

USAJILI MPYA

Kwenye dirisha la usajili msimu huu Polisi Tanzania imesajili wachezaji wapya 11 kutoka katika timu tofauti beki wa kati, Sosteneth Idah, Blanchard Ngabonziza, Salumu Kipemba na Iddy Kipagwile.

Wachezaji wengine, James Mwasote, Salum Chuku, Hassan Kapona, Fredy Tangalo, Hamisi Kanduru, Ambrose Awio na Jamal Mtegeta katika orodha hii nyota hao wameshindwa kuanza katika ubora wao.

Kumekuwa na changamoto katika eneo la ulinzi ambalo wanacheza, Idah, Ngabonziza, Mwasote, Kapona na Chuku pengine ndio maana imekuwa katika orodha ya timu iliyoruhusu mabao mengi hadi sasa ikifungwa saba.

Katika eneo la kushambulia katika michezo mitano ya ligi Polisi Tanzania imefunga mabao manne licha ya uwepo wa nyota mpya kama, kipagwile, Awio, Kanduru na Mtegeta ambaye muda mwingine hutumika kama kiungo.

KIONGOZI

Ofisa habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro anasema upya wa wachezaji unawaathiri lakini watakaa sawa.

Chanzo: Mwanaspoti