Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania Yamfuta Kazi Kocha Wao Joslin Sharif

Kocha Polisi Tanzania Joslin Sharif Bifubusa (katikati)

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Polisi Tanzania imemtimua Kocha wake Joslin Sharif Bifubusa na kulivunja bench lote la ufundi , kutokana na kutoridhidhshwa na mwenendo wa timu hiyo.

Joslin ambaye aliajiriwa kuwa Kocha mkuu wa timu hiyo Julai 26 mwaka huu, amedumu kwa kipindi cha miezi mitatu huku ujio wake klabuni hapo kutobadilisha chochote kwa Polisi.

Polisi Tanzania msimu huu wameanza vibaya sana licha ya kusajili wachezaji kadhaa na wengine kutimka, ambapo mpaka sasa ndio wanaoshikilia mkia kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC wakiwa nafasi ya 16.

Wamecheza michezo saba na kati ya hiyo michezo saba hakuna mchezo walioshinda, wamepata sare moja na wamepoteza michezo mitano na pointi zao mbili kibindoni. Kesho watakuwa nyumbani kuwakaribisha Namungo kwenye mchezo wao wa raundi ya 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live