Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kuipeleka Singida Big Stars Karatu

Polisi TZ Uwanja Polisi Kuipeleka Singida Big Stars Karatu

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa ligi kuu kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Singida Big Stars sasa utapigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu, Arusha.

Sababu ya mabadiliko ya uwanja ni baada ya kufungiwa kwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao ulikuwa ukitumiwa na Polisi Tanzania kama uwanja wao wa nyumbani.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa watautumia uwanja huo kwa mchezo dhidi ya Singida Big Stars.

“Kikosi kinaendelea na maandalizi ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya Singida Big Stars, utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu ambazo ni muhimu kwetu.

“Baada ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid kufungiwa kwa sasa tutautumia uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu kwa ajili ya mchezo huo.

“Tayari marekebisho ya uwanja wetu wa nyumbani wa Ushirika yamekamilika tunachosubiri kwa sasa ni ruhusa kutoka bodi ya ligi hivyo tuna imani baada ya kumalizika kwa mchezo ujao mechi nyingine tutacheza Moshi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live