Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pogba ndio basi tena Man United

Paul Pogbaaaaa Paul Pogba akitoka kwa Maumivu mechi dhidi ya Liverpool

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United Ralf Rangnick amesema huenda kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba asicheze mechi yoyote msimu huu kutokana na majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool.

Pogba mwenye umri wa miaka 29, alitoka nje ya uwanja dakika ya 10 wakati Liverpool wakiongoza goli moja kwa bila bao la Luis Diaz hata hivyo majereha yalionekana kuwa madogo lakini taarifa zinasema atakuwa nje kwa angalau wiki nne.

United wamebakiwa na mechi tano za EPL kuanzia mechi ya Jumamosi dhidi ya Arsenal ambapo pia kwenye mechi hiyo huenda Cristiano Ronaldo, Raphael Varane na Scott McTominay wakarejea uwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live