Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pogba hati hati kuikosa michuano ya Kombe la Dunia

Paul Pogba Upasuaji Paul Pogba

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Juventus Paul Pogba leo kupitia mitandao yake ya kijamii amaechapisha video ya kuthibitisha kufanyiwa upasuaji baada ya kusumbuliwa na jeraha la goti kwa wiki kidhaa sasa.

Pogba mwenye miaka 29, alipata majeraha ya goti akiwa nchini Marekani kwenye michezo ya Pre-season, na awali ilibidi afanyiwe upasuaji nchini Marekani kabla ya klabu hiyo kuamua kumtafutia mshauri wa afya wa kuangalia ni namna gani atafanyiwa upasuaji ili aweze pona haraka.

Awali alikutana na mshauri nchini Ufarasana kwa ajili kuangalia uwezekano wa uchaguzi upi bora kwa ajili ya upasuaji wake huku kukiwa njia mbili za kuweza kutibu jeraha lake ambapo awali ni kuponya kidonda na ya pili ndio upasuaji wa kuondoa “meniscus”.

“Natumai nyote mko vizuri, mimi ni mzima namshukuru mungu upasuaji umenda vizuri. Natarajia kurudi hivi karibuni, ningependa kuwashukuru ninyi nyote kwa jumbe zenu, hamasa yenu na kujua kwamba niko sawa kiakili licha mashaka yote na majeraha.

“Pamoja na matatizo yote nainua kichwa changu juu, sipo peke yangu nipo na mungu wangu wangu, nyote nawashukuru jumbe zenu zote, ushirikiano wenu wote ambao nimeouna kwenye mitandao ya kijamii.

“Tutarudi kwa kishindo hivi karibuni na natumai itakuwa sawa natuma salamu zangu kwenu na kuwaaga.” Alichapisaha video kwenye mtandao wa Twitter

Upasuaji huo unatajwa huenda ukamkosesha nyota huyo kushiriki michuano ya Kombe la Dunia inayoanza mwishoni mwa mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live