Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pogba dimbani wikiendi hii

Skysports Pogba Paul Juventus 6083136 Paul Pogba

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Juventus Paul Pogba yuko tayari kurejea ndani ya klabu hiyo siku ya jumapili kuitumikia klabu hiyo katika mchezo dhidi ya Sampdoria baada ya adhabu yake kumalizika.

Kocha Juventus Massimiliano Allegri amethibitisha Pogba yupo kwenye mipango yake na ataitumikia klabu hiyo siku ya jumapili katika mchezo wa ligi kuu nchini humo Serie A baada ya kusimamishwa kutokana na makosa ya kinidhamu ambayo hayakuwekwa wazi na klabu hiyo.

Kiungo Paul Pogba hakua sehemu ya timu katikati ya wiki ambapo klabu ya Juventus ilimenyana na klabu ya Feriburg katika mchezo wa hatua ya 16 bora bora jombe la Europa League, Lakini kiungo huyo atakuepo sehemu ya kikosi hicho kesho ambapo miamba hiyo itakapomenyana na kalbu ya Sampdoria.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akiandamwa na majeraha ndani ya klabu hiyo mara kwa mara tangu aliporejea klabuni hapo akitokea Manchester United dirisha kubwa lililopita, Kutokana na majeraha hayo yamemfanya kukosa nusu ya msimu ndani ya klabu hiyo pamoja na michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Klabu ya Juventus leo itahitaji alama tatu ili kuendelea kufukuzia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao, Baada ya kupoteza mchezo wa ligi hiyo wikiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya As Roma huku Pogba nae atacheza mchezo wake wa pili wa Serie A msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live