Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pogba auza jumba lake la kifahari

Pogba 6809701 Pogba auza jumba lake la kifahari

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo, Paul Pogba ameirudisha tena sokoni nyumbani yake yenye thamani ya Pauni 4 milioni akijaribu kupata chochote baada ya kufungiwa kucheza soka kwa kipindi cha miaka minne.

Staa huyo wa zamani wa Manchester United, ambaye alipimwa mwaka jana na kukutwa ametumia dawa zinazopigwa marufuku michezoni, alinunua nyumbani hiyo, yenye uwanja mdogo wa soka ndani kwa Pauni 3 milioni mwaka 2016.

Alikuwa anapangisha nyumba hiyo iliyopo Hale Barns, Cheshire, lakini alishusha kodi kutoka Pauni 27,500 kwa mwezi hadi Pauni 18,000 baada ya kushindwa kupata mpangaji.

Na sasa jumba hilo lililojengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa futi za mraba 7,400 limerudishwa tena sokoni. Jumla hilo lina mambo kibao yanayovutia wengi. Imeweka pia geti baada ya kiungo huyo kuvamiwa na wezi mwaka 2022, wakati familia yake na watoto walipolala juu.

Pogba alikuwa akiitumia Man United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Atletico Madrid na kuwahi kurudi nyumbani baada ya tukio.

Kiungo huyo wa Juventus alifungiwa soka Februari mwaka huu baada ya kufeli vipimo vya matumizi ya dawa zinazopigwa michezoni.

Juventus imesitisha mkataba wake jambo ambalo linatishia kama mchezaji huyo ataonekana tena uwanjani. Staa huyo yupo kwenye  hatari ya kupoteza wadhamini wake, ikiwamo dili la Adidas linalomwingizia Pauni 31 milioni.

Pogba, ambaye amepinga kufanya kosa, kwa sasa anaishi na mkewe mrembo Zulay huko Italia kwenye jumba la Cristiano Ronaldo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live