Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pogba apata mtoto wa tatu

Pogba Mtre Pogba apata mtoto wa tatu

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paul Pogba ametumia mtandao wake wa Instagram kutujuza taarifa njema za kupata mtoto wa tatu, akisema kuwa "ana furaha sana kuwa baba wa watoto watatu".

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United ali-share picha mbalimbali akiongea na mkewe kupitia Facetime wakati akielekea Hosptali huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka "Al hamdulillah mwanakaya mpya wa familia ya Pogba amewasili, najivunia sana Malkia wangu, nimefurahi sana, #babawatatu".

Ujio wa binti yake unamfanya Pogba kuwa na watoto watatu wakiwemo Labile aliyezaliwa mwaka 2019 ikiwa ni mwaka ambao kiungo huyo wa Juventus alifunga ndoa, pamoja na Keyaan aliyezaliwa mwaka 2020.

Hivi sasa Pogba anasumbuliwa na majeraha yaliyosababisha mwanzo mgumu wa kiungo huyo wa Juventus ya nchini Italia aliyojiunga nayo baada ya kuachana na miamba ya England Klabu ya Manchester United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live