Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pogba: Sijawahi kutumia madawa, Nitakata rufaa

Paul Pogba Asalia Juve Paul Pogba

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Juventus Paul Pogba leo hii baada ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 4 kwa kosa la kutumia madawa ya kuongeza nguvu amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa uamuzi wa mahakama sio sahihi.

Pogba ameeleza kuwa ameshitushwa na taarifa hizo pia ameumia sana kuona akisimamishwa kuendelea na taaluma yake aliyoipambania kwa muda mrefu.

Pobga amefunguka kwamba akiwa huru ataeleza kila kitu kilichotokea lakini anaamini kwamba hajawahi kutumia kabisa dawa za kuongeza nguvu na anadai kwamba kama mchezaji anayefahamu vizuri maadili ya soka hawezi kabisa kutumia kitu chochote ili kuongeza nguvu akiwa uwanjani.

Sambamba na hayo Pogba ameahidi kukata rufaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live