Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettiono pendekezo namba moja Man United

Skysports Mauricio Pochettino 5523923 Mauricio Pochettino, Pendekezo nama moja la kumrithi Ole Gunner Solskjaer

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati vungu vugu la kutakiwa kwa Mwalimu mpya ndani ya kikosi cha Man United likizidi kupamba moto.

Taarifa zinaeleza kuwa Kocha wa sasa wa klabu ya PSG, Mauricio Pochettino ndie anaependekezwa kuchukua kibarua hicho pale atakapofukuzwa Ole Gunner Solskjaer.

Solskjaer ni kama haelewi hatma yake kwa sasa kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu ndani ya Manchester United.

Tukio la kupigwa magoli 5-0 wikiendi iliyopita kutoka kwa Liverpool ndio kama limeamsha zoezi hili licha ya kuwa viongozi ndani ya United wana nia ya kumpa nafasi ya kukinoa kikosi hicho, lakini matokeo ndio yanayowasukuma kutazama mbele zaidi kutazama mbadala wake.

Kocha wa zamani wa Man United, Mkongwe Sir. Alex Ferguson anasemekana kumkingia kifua na kusisitiza apewe nafasi na muda huenda akabadilisha hali ya mambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live