Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino atupiwa virago Chelsea, Man United yatajwa

Mauricio Pochettino 4842395 Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea imethibitisha kuachana na kocha wake Mauricio Pochettino kwa makubaliano ya pande zote mbili huku akitajwa kutua Manchester United.

Pochettino (52) alijiunga na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu alipitia wakati mgumu katikati ya msimu huu baada ya timu hiyo kupata matokeo ya kusuasua ingawa mwishoni alifanya vizuri.

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo inasema, “Chelsea FC inathibitisha kuwa tumefikia makubaliano ya kuachana na Mauricio Pochettino kwa makubaliano ya pande zote mbili.”

Kocha huyo ambaye mwishoni mwa msimu huu ameonekana kuinasua timu hiyo ambayo, Machi mwaka huu ilikuwa nafasi ya 12 kwenye msimamo, mpaka anaondoka ameiacha ikiwa nafasi ya sita.

Makocha wasaidizi Jesus Perez, Miguel d'Agostino, Toni Jimenez na Sebastiano Pochettino nao pia wameingia kapu moja na Pochettino.

Taarifa zinasema kuwa United ambayo inaweza kuachana na kocha wake Eric ten Hag muda wowote kuanzia sasa inataka kumchukua kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur.

Kocha wa Sporting Lisbon, Rúben Amorim anatajwa kuchukua nafasi ya Pochetinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live