Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino anapiga hesabu kunasa huduma ya beki Harry Maguire kabla dirisha hili la kiangazi halijafungwa.
Staa huyo wa kimataifa wa England 30, anaweza kuachana na Manchester United dirisha hili baada ya kuvuliwa unahodha na kocha Erik ten Hag ikiwa na maana hayupo kwenye mipango ya Ten Hag.
Ishu ya Pochettino kuvutiwa na Maguire ilifichuliwa na Danny Rose, mmoja wa wachezaji wake wa zamani, ambaye alisema: “Nakumbuka tulicheza na Hull uwanjani White Hart Lane (Desemba 2016) na tulishinda 3-0. Mauricio alikuwa kocha wetu na Harry alikuwa kila sehemu.
Spurs nadhani walihitaji saini yake. Poch alionekana wazi kuhitaji saini yake. Nilipokuwa nafanya naye mazoezi kwenye kikosi cha England, ilikuwa ngumu sana kupata mpira kutoka kwake. Ni mzuri kiasi hicho.”