Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema sio jukumu lake kutatua hatima ya Mshambuliaji Romelu Lukaku ambaye mpaka sasa hakijaeleweka Stamford Bridge.
Lukaku aliondolewa katika kikosi cha Chelsea na anafanya mazoezi na timu ya vijana wenye umri wa miaka 21 baada ya kuweka wazi kuwa anataka kuondoka baada ya kurejea London, kufuatia mkopo wake kumalizika Inter Milan.
Hadi sasa hakuna timu iliyojitokeza kuonyesha nia ya kumsajili ikiwa imebaki wiki moja dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kufungwa.
Lukaku alijiharibia alipoonyesha nia ya kujiunga na Juventus huku Inter Milan ikichukizwa na nidhamu mbovu aliyoonyesha.
Awali, Inter Milan ilikuwa na nia ya kumsajili jumla, lakini kutokana na mpango wake huo ikaamua kuachana naye na Lukaku akarejea Stamford Bridge.
Baada ya kurejea London, Chelsea ilimtaka kujiunga na moja ya timu kútoka Saudi Arabia, lakini aligoma.
Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa Lukaku ambaye alisajiliwa kwa rekodi ya usajili wa Pauni 9.5 milioni, Pochettino alisema: “Kama ishu za kusuluhisha maslahi ya wachezaji sihusiki. Mchezaji anatakiwa kuonana na viongozi kujadili na kufikia muafaka. Nimechanganyikiwa kutokana na ishu ya Lukaku inavyokwenda.
Mimi nahusika na mambo ya usajili wa wachezaji na kujenga kikosi, lakini kuhusu mambo mengine sihusiki kabisa. Nafahamu ishu ya Lukaku ilivyokuwa na nguvu, na naamini suluhu itapatikana.