Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino aanza kumfikiria Marc Cucurella

Image 43 1140x640.png Pochettino aanza kumfikiria Marc Cucurella

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino, anapanga kumjumuisha Marc Cucurella kwenye kikosi cha kwanza ambacho bado kinatafutwa msimu huu.

Cucurella aliwasili Stamford Bridge kutoka Brighton & Hove Albion msimu uliopita wa majira ya joto kwa Pauni Milioni 55, huku kukiwa na nyongeza ya ada hadi Pauni Milioni 62.

Kama wachezaji wenzake wengi wapya, Mhispania huyo alitatizika Chelsea ilipomaliza nafasi ya 12, ikipitia kwa makocha wanne kabla ya mwisho wa msimu wa 2022/23.

Baada ya kutochaguliwa na kocha mpya Pochettino kwa mechi tatu za ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu, imeripotiwa kuelekea mwisho wa dirisha la usajili la majira ya joto kwamba Manchester United walikuwa wameanzisha mazungumzo na Chelsea kuhusu kumnunua kwa mkopo Cucurella.

Hata hivyo, Cucurella alitajwa katika kikosi cha kwanza cha ‘The Blues’ kwenye ushindi wa mechi ya Carabao raundi ya pili dhidi ya AFC Wimbledon.

Baadae Man United ikachagua kumsajili Sergio Reguilon kwa mkopo kutoka Tottenham Hotspur badala yake.

Mechi nyingine pekee ya Cucurella msimu huu ni ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu yake ya zamani ya Brighton katika raundi ya tatu ya Kombe la Carabao juma lililopita na bado hajacheza dakika hata moja kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Chanzo: Dar24