Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino: Tulistahili alama 3

Mauricio Pochettino Managing Paris Saint Germain In The Champions League Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino mara baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Arsenal

"Ni kweli tumeumia lakini hatuwezi kutazama tu dakika za mwisho. Kulikuwa na mabadiliko mengi chanya. Tulikuwa timu bora."

"Tumepoteza alama mbili kwa namna ambayo usingetamani kuzipoteza, lakini kwa namna tulivyocheza dhidi ya timu ambayo msimu uliopita ilikuwa inashindania kushinda taji la ligi kuu tumepata mengi mazuri ya kujivunia. Tulionyesha soka zuri."

"Tulikuwa washindani, tulistahili kupata zaidi na tunatakiwa kuamini kwenye hiki tunachokifanya kwasababu mambo mazuri yatakuja. Ninapenda vile wachezaji wanajitazama kwasasa, wameumizwa sana na kukosa ushindi. Ninapenda nione hali kama hiyo. Lakini tunatakiwa kuendelea kufanya kazi, tupo kwenye njia sahihi."

"Tulihitaji kubadilisha aina na mbinu ya namna ya kushambulia. Tulihitaji kuwa na ubora mkubwa wa Cole Palmer na Conor Gallagher kwenye eneo la katikati ili kuwazuia mabeki wa kati wasiweze kujiamini na kusogea mpaka eneo la kiungo."

"Kisha kuwatumia Sterling na Mudryk kutengeneza mazingira ya kuzuiwa mmoja dhidi ya mmoja. Nimefurahishwa sana na kiwango cha Palmer na Gallagher."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live