Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino: Palmer ndio mpigaji wa Penati Chelsea

Poch Pena Pochettino: Palmer ndio mpigaji wa Penati Chelsea

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Chelsea, Mauricio Pochettino amechukizwa na kitendo cha wachezaji klabu hiyo Nickolas Jackson na Noni Madueke kuonekana kugombania nafasi ya kupiga penalti dhidi ya Everton kabla ya Cole Palmer kuchukua mpira na kufuingia Chelsea bao la tano katika dimba la Stamford Bridge.

Pochettino ameondoa utata huo na kubainisha kuwa Cole Palmer ndiye mpigaji wa penalti klabuni hapo na kusema kitendo kilichotokea ni aibu na utoto hivyo amewaonya wachezaji wake kuwa hatarajii kuona kitendo hicho.

“Palmer ndiye mpiga penalti. Haitatokea tena, hawawezi kuwa kama watoto tena”.

“Ni aibu. Niliwaambia wachezaji hii ni mara ya mwisho kukubali tabia ya aina hii. Huu sio mzaha”.

“Tena, naweka wazi kabisa. Cole Palmer ndiye mpigaji wa penalti”. Pochettino.

Mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kuitandika Everton jumla ya magoli 6-0 huku Cole Palmer akifunga magoli manne na kukwea kileleni mwa mbio za kuwania kiatu cha dhahabu Ligi Kuu England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live