Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino: PSG Hatafungwa Kw asababu ya Referee

Maurico Pochettino 20 Mauricio Pochettino

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Paris Saint Germain Mauricio Pochettino amekataa kutoa lawama kwa mwamuzi alichezesha mchezo wao dhidi ya Nantes siku ya jumamosi na kupoteza kwa goli 3-1 kwenye dimba la Stade de la Beaujoire.

Nantes walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu hasa kwenye kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata goli tatu zote ambazo zilifungwa na Randal Kolo Muani, Quentin Merlin na Ludovic Blas

Wakati akihojiwa na waandishi Pochettino alinukuliwa akisema, “tulifanya shambulio letu la kwanza kupitia Juan Bernat lakini walitufunga kwenye shambulio lililofuata, tulijaribu mara mbili kwenye muda wa majeruhi, tulifanya mashambulizi mazuri, lakini hatukuwa na udhibiti mzuri wa nafasi ya ulinzi hii ni pamoja na makosa mengi tuliyoyafanya.

“Inabidi tutenganishe hili, Hatukupoteza kwa sababu ya referee, naweza kuelewa shinikizo la wachezaji wangu na mkurugenzi, ungeweza kurudia mchezo, lakini haimaanishi kuwa ndio sababu ya kupoteza.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live