Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino: Nkunku bado kidogo

Christopher Nkunku Inury Pochettino: Nkunku bado kidogo

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amegoma kumharakisha Christopher Nkunku kurudi uwanjani akidai anataka akirudi akiwa fiti asilimia 100.

Chelsea haiko tayari kuchukua hatari yoyote baada ya Nkunku kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu tangu alipoumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund baada ya kugongwa na Mats Hummels.

Sasa kwa mujibu wa kocha huyo mashabiki wasitarajie kumuona Nkunku hadi atakapokuwa fiti na wanaendelea kufuatilia maendeleo yake.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa bado hajacheza mechi yake ya kwanza ya ushindani tangu aliposajiliwa akitokea RB Leipzig, baada ya kupata jeraha la goti Julai mwaka huu.

Wakati Pochettino bado hajatoa taarifa mpya kuhusu hali ya mshambuliaji huyo wa zamani wa RB Leipzig, gazeti la The Standard linadai kuwa mchezaji huyo huenda akaungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United itakayochezwa Jumamosi.

Kabla ya mechi ya dhidi ya Manchester City mwezi uliopita, Pochettino alifichua mazungumzo yake na Mfaransa huyo kwamba alimwambia kocha wake anatazamia kurejea uwanjani baada ya mapumziko ya ligi kupisha mechi za kimataifa mwezi huu.

Nyota mwingine wa Chelsea, Wesley Fofana anaweza kuwa njiani kurejea mazoezini baada ya kupata jeraha mwezi Julai. Beki huyo alidokeza atarejea kupitia akaunti yake Instagram.

Wakati huo huo, kiungo mpya aliyesajiliwa katika dirisha lililopita, Romeo Lavia anatarajiwa kurejea wiki hii na huenda akacheza mechi yake ya kwanza akiwa na uzi wa Blues.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live