Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pochettino: Chelsea tamu siku zote

Mauricio Pochettino Managing Paris Saint Germain In The Champions League Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesisitiza mashabiki wasishangae kiwango cha timu yao baada ya kuifunga Brighton na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu michuano ya Ulaya, kwani hivyo ndivyo walivyokuwa wakicheza tangu mwanzo wa msimu ila hawakuwa wanapata matokeo tu.

Chelsea ambayo imefikisha pointi 60 ambazo zimewaweka katika nafasi ya sita ya kufuzu UEFA Conference League, inahitaji pointi moja tu katika mchezo wao wa mwisho wa ligi ili isishushwe na wapinzani wao Newcastle na Manchester United.

“Tumekuwa tukicheza hivi tangu mwanzo wa msimu, utofauti ni kwamba hatukuwa tunashinda mechi kama ilivyo sasa, kwangu mimi Chelsea ni timu nzuri, shida ni watu huwa wanaangalia matokeo tu,” alisema Pochettino.

Msimu uliopita Chelsea ilimaliza nafasi ya 12, lakini msimu huu katika mechi nne za mwisho zote imeshinda ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwao tangu mwaka 2022 na ipo katika mazingira mazuri ya kumaliza nafasi ya sita.

Baada ya kushinda mchezo wao muhimu uliowapa nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Ulaya Pochettino aliwapongeza wachezaji wake na akazungumzia pia kadi nyekundu aliyopewa beki Reece James baada ya kumkanyaga Joao Pedro akisema imewaumiza kwa sababu beki huyo alikuwa katika kiwango bora na jambo la huzuni ni ataenda kuikosa mechi ya mwisho ya msimu.

Chanzo: Mwanaspoti