Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Plujm awachimba mkwara Polisi

Ujm Singida Md.jpeg Plujm awachimba mkwara Polisi

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Singida Big Stars, Hans van der Pluijm amesema anaiheshimu timu ya Polisi Tanzania na anaamini mchezo wao leo kwenye Uwanja wa Black Rhino, uliopo Karatu utakuwa mgumu kutokana na timu zote jinsi zinavyocheza.

Akizungumza, Pluijm alisema anaendelea kukiandaa kikosi chake huku akijua kabisa utakuwa ni mchezo mgumu kwa sababu timu zote zina vijana wapambanaji.

“Hii Polisi sio timu ya kuidharau kwa sababu ilimfunga Namungo na ilicheza vizuri, mchezo wake uliopita. Nilipata muda wa kuwaangalia kwenye kipindi cha pili, wanacheza vizuri sana kwahiyo naheshimu sana wapinzani wangu,” alisema Pluijm na kuongeza;

“Wachezaji wangu ni wapambanaji kwahiyo naamini ndani ya dakika 90 zote watajitoa kuhakikisha timu inapata ushindi.”

Pluijm alipogundua kama uwanja wa mchezo huo umebadilishwa kutoka Sheikh Amri Abeid na kwenda Black Rhino alisema hakuna tatizo lolote kwa sababu viwanja vyote hivyo ni vya nyasi za asilia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live