Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pluijm kuwaburuza Yanga FIFA

Hans Van Der Pluijm.png?fit=602%2C439&ssl=1 Hans Van Der Pluijm

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amethibitisha kuwa kuna uwezekano mkubwa akaifungulia mashitaka klabu ya Yanga kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘FIFA’ kuhusiana na madai ya stahiki zake.

Inaelezwa kuwa kocha huyo anawadai Yanga kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 115 za Kitanzania.

Pluijm, aliiongoza Yanga kama kocha mkuu kwa vipindi viwili tofauti kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, huku pia akiwahi kushika nyazifa nyingine ndani ya klabu hiyo.

“Taarifa za mimi kuwa kwenye mpango wa kuwapeleka Yanga FIFA ni za kweli, lakini nisingependa kuzungumza sana kuhusu suala la kesi hii kwa sasa, kwa kuwa kuna wawakilishi wangu ambao wako Dar es Salaam kwa sasa wanashughulikia kesi hii". amesema Pluijm.

JItihada zilizofanyika kuwapata viongozi wa Yanga,zilifanikiwa kumpata Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli.

“Taarifa za kudaiwa na kocha Hans zinapaswa kuwekwa sawa kwa kuwa ni kweli alikuwa akitudai lakini tayari suala hili lilishafanyiwa kazi” amesema Bumbuli

Chanzo: globalpublishers.co.tz