Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate FC, Hans Pluijm inaelezwa anaweza kupangiwa nafasi nyingine ya kuhudumu ndani ya Klabu hiyo baada ya taarifa kueleza kuwa Singida Fountain Gate FC wapo kwenye Mpango wa kumuajiri Kocha Mkuu mwingine.
Hans Pluijm anamaliza Mkataba wake na Singida Fountain Gate FC mwezi ujao na inaelezwa ataendelea kusalia Klabuni hapo kama Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo.
Hussein Massanza amesema: "Ni kweli Hans Pluijm anamaliza mkataba wake mwezi ujao ila hatuna tunachomdai maana amefikia malengo ya timu yetu kwa kutifikisha Top Four.
"Kukusu Kocha mwingine bodi ndio itaamua kutokana na malengo ya timu, tumeona kuna timu zimewaaga watu wao so usishangae hata huyo Cedric Kaze ambae inaelezwa amemaliza kandarasi yake Yanga SC bodi ikimpendekeza akajiunga na sisi Singida Fountain Gate FC," amesema Afisa Habari wa Singida Fountain Gate FC.