Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pluijm azivimbia Simba, Yanga

Hans Van Der Pluijm.png?fit=602%2C439&ssl=1 Kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amewapongeza nyota wa timu hiyo kwa kuifunga Namungo mabao 3-0, huku akizivimbia Simba, Yanga na Azam kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara akisema anaamini kitaeleweka mbele ya safari.

Singida ikicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Liti, Singida ilipata ushindi wake kupitia nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Meddie Kagere, Amissi Tambwe na Said Ndemla na kuifanya ifikishe pointi 27 ikijikita nafasi ya nne baada ya mechi 14, huku Namungo ikisalia nafasi ya tisa na pointi 18.

Pluijm aliyewahi kuzinoa Yanga na Azam FC alisema wachezaji wake walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi ambazo walizitumia hivyo anawapongeza kwa kazi nzuri na anaona uelekeo kwa timu hiyo kuchuana na vigogo baada ya kuanza vyema mwanzoni mwa msimu kisha kuyumba akiamini kila kitu sasa kipo sawa kwao.

“Tunashukuru kwa ushindi huu, unaongeza morali kwa wachezaji katika kushindana na timu nyingine, matokeo ya mechi zilizopita yaliturudisha nyuma, ila kwa sasa kazi imeanza.

“Nawapongeza sana wachezaji kwa walivyojitoa na kupata ushindi huu muhimu nyumbani,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi, huku nahodha wa timu hiyo, Deus Kaseke akisema ulikuwa mchezo mzuri wanashukuru kwa kupambana na kupata ushindi mnono.

Kocha Msaidizi wa Namungo, Shadrack Nsajigwa alisema walifanya makosa kipindi cha pili na wapinzani wao waliwaadhibu na wanaenda kujipanga kwa mechi ya kiporo dhidi ya Yanga itakayopigwa Uwanja wa Majaliwa, mjini Ruangwa Lindi Jumatano ijayo. Siku hiyo Singida nayo itamaliza kiporo chake na Coastal Union.

“Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri, ila hatukutumia nafasi, lakini wachezaji waliyumba kwenye kipindi cha pili na kuwapa nafasi wenyeji kupata mabao yaliyoibeba.”

Chanzo: Mwanaspoti