Kocha wa Singida Big Stars,Hans Pluijm aleza namna Kocha mpya wa Yanga atakavyopata changamoto kubwa msimu ujao kutokana na deni kubwa lililoachwa na mwalimu aliepita Nasreddine Nabi.
Yanga ambayo ilimalizana na Kocha Nabi mara baada ya kumalizika kwa msimu uliokuwa na mafanikio makubwa kwao kwa kuwa washindi wa pili katika fainali ya Kombe la Shirikisho,kubeba Kombe la FA na Ubingwa wa Ligi Kuu bila kusahau Ngao ya Jamii.
Pluijm ambae aliwahi kuitumikia Yanga na Azam pia, alimzungumza na Mwanaspoti na kusema kocha ajae atapata changamoto kwani kufanikiwa kama mwalimu aliyepita kwake itakuwa ngumu kwani ufanyaji kazi wao ukotofauti.
Aidha alisema wakati Nabi anaingia Yanga alikutana na wachezaji bora wenye uwezo na uzoefu wa kucheza hivyo hakuwa na haja ya kufundisha namna ya kucheza bali akili na uwezo wa kufunga.
Alieleza kuwa kocha huyo wa Yanga alilenga kujenga wachezaji katika kutumia nafasi vizuri na kuwatengeneza kuwa bora ndio maana alifanikiwa kuwa na kikosi kinacholeta matokeo bila kuwa na tegemezi kwani wote walikuwa bora.
"Kila Kocha anakuwa na namna yake ya kufundisha na wachezaji pia wanaweza kupata ugumu wa kufuata mfumo mpya hivyo sio kazi rahisi sana atakayokuwa nayo mwalimu mpya wa Yanga."
"Nabi alikuwa Kocha mwenye heshima na alijua kusoma haraka aina ya wachezaji aliokuwa nao hivyo akamaliza msimu kwa kuwa na viungo bora na ushindi ambao umeacha alama nzuri kwake na timu kwa ujumla," alisema Pluijm.
Kocha huyo wa Singida Big Stars, alimuelezea kocha Nabi aliyeitumikia Yanga kwa kipindi cha misimu miwili mfululilizo na kwa mafanikio makubwa kuwa ni mfano wa kuigwa.