Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pluijm: Siihofii Yanga ng'o

Hans De Pluijm Pluijm: Siihofii Yanga ng'o

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuifunga KMKM, Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans van Pluijm amesema haihofii Yanga kwenye mchezo unaofuata, zaidi amefurahia kupangwa kundi moja kwa sababu anapenda mechi kubwa.

Singida Big Stars, katika michuano hiyo ya Mapinduzi wako kundi B, pamoja na timu ya Yanga na KMKM ya Visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm alisema amefurahishwa na morali ya wachezaji wake kwenye mchezo wa kwanza na kuweka wazi kuwa wakiendelea hivyo anaiona timu hiyo ikitinga fainali na kutwaa taji.

Singida juzi walifanikiwa kuwachapa KMKM mabao 2-0 kwenye mchezo wao wa kwanza wa michuano hiyo.

“Kupangwa kundi moja na Yanga ni furaha kwangu napenda kucheza na timu kubwa kwasababu zinatoa ushindani wa kweli na mimi nimekiandaa kikosi kushindana mchezo wetu na wao natarajia ushindani,” alisema na kuongeza;

“Makosa tuliyoyafanya kwenye Ligi Kuu Bara kwa kukubali kipigo cha mabao mengi hatutarajii kuyarudia huku kwasababu tunacheza mechi za mtoano na lengo letu ni kufika mbali, tunataka pointi mechi zote.” alisema.

Alisema lengo lao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa na hili ni lengo la kila kocha aliyepeleka timu kwenye mashindano hayo hivyo watahakikisha wanapambana kupata matokeo kwenye kila mchezo ili waweze kufikia malengo.

Januari 6, Yanga wataingia uwanjani kuvaana na Singida ukiwa ni mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.

KAGOMA, KAZIDI FRESH Pluijm akizungumzia mastaa wake wapya kwenye kikosi chake alisema amefanya machaguo sahihi sasa anaona matunda yake kutokana na namna walivyocheza vizuri dhidi ya KMKM.

“Yufuph Kagoma ni kiungo mzuri anajua kucheza kwenye nafasi anakaba na kutengeneza mashambulizi ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kukupa kila kitu uwanjani,” alisema na kuongeza;

“Sio vizuri kutaja jina la mchezaji mmoja mmoja kutokana na kucheza kwa ushirikiano lakini hata huyo Fancy Kazidi, amefanya kazi kubwa alikuwa anapanda na kushuka alifanya majukumu mengi uwanjani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live