Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pitso amtaka nyota wa zamani Afrika Kusini kuwa Kocha

Pitso Wants Pitso amtaka nyota wa zamani Afrika Kusini kuwa Kocha

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa klabu ya Mamelodi Sundowns na Al Ahly ya Misri Pitso Mosimane amemtaka mchezaji wa zamani wa Mamelodi Sundowns na timu ya Taifa ya Afrika Kusini Katlego Mphela kusomea ukocha akiamini atakuwa kocha bora kama ilivyo kwa Rulani Mokwena.

Katlego Mphela alistaafu kucheza mpira mwaka 2019 na kuhamia biashara ya kuuza magari, jambo ambalo limemfurahisha pia Pitso huku akiamini anaweza kuendelea na biashara hiyo huku akifanya kile anachokipenda kwa maana ya soka.

Pitso amesema atamsaidia kwa hali zote ili ahakikishe anapata sifa za kuwa kocha bora. Pitso anataka sana wachezaji wa zamani wa Afrika Kusini warejee kwenye kuufundisha.

Kwetu vipi, ni mchezaji gani wa zamani unatamani arejee, awe kocha na unaamini atafanya vizuri?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live