Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pitso akalia kuti kavu Saudi Arabia

Pitso Mosimane Al Wahda FC Kocha Pitso Mosimane

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge na klabu Abha FC ya nchini Saudi Arabia inayoshiriki ligi ya Saudi Pro League, kocha huyo amekuwa na upepo mbaya wa vipigo tangu ajiunge na klabu hiyo ambapo jana amepoteza tena kwa kufungwa magoli 5-0 dhidi ya Al Shabaab.

Msimu huu Pitso ameiongoza klabu hiyo kwenye jumla ya michezo 23 kwenye mashindano yute aliyoshiriki huku akishinda michezo 11, sare 3 na kupoteza michezo 9 na kwenye ligi ya Saudi Pro League anashika nafasi ya 15 ambayo ni ya 4 kutoka mwisho.

Kwenye michezo 5 ya mwisho Pitso amepoteza michezo 3, sare 1 na kushinda 1 huku akipokea kipigo cha magoli 8-0 dhidi ya Al Nasr na akipoteza tena jana kwa mabao 5-0 dhidi ya Al Shabaab.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live