Kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly Pitso Mosimane ambae kwa sasa anafundisha klabu ya Al Ahli inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Saudi Arabia kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika.
"Mtindo wa uchezaji soka wa timu za Afrika kisini, ni mgumu kwa timu za Afrika Kaskazini, haswa timu zinapocheza kwa majigambo na kujiamini.
Timu za SA zimewahi kushinda mataji ya bara na zitaendelea kufanya hivyo. Mtu yeyote anayezidharau, atakuwa katika hatari yake mwenyewe. Hawataacha kushangaza.
Timu za SA hupoteza baadhi ya michezo, na ni kawaida katika soka, lakini sasa ni wakati wa kuelewana na kuamini kuwa inawezekana 2023 ni Mwaka! Viva SA football," ameandika Pitso Mosimane kwenye Twitter.
Mpaka sasa Afrika Kusini imebakiza timu mbili kwenye michuano ya Vilabu barani Afrika ambazo ni Mamelodi Sundowns (Klabu Bingwa) ambao watacheza na Wydad kwenyw nusu fainali ya michuano hiyo na Kwa upande wa kombe la Shirikisho wapo Malumo Gallants ambao watacheza nusu fainali na Yanga.