Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pisi kali za Ligi Kuu England

Mateo Kovacic Pisi kali za Ligi Kuu England

Mon, 29 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wanasema nyuma ya mwanamume mwenye mafanikio amesimama mwanamke. Na hilo lilithibitishwa na Manchester City, baada ya kufanikiwa tu kubeba taji la Ligi Kuu England, mastaa wake waliamua kuwachukua wake zao na kwenda kujipongeza.

Lakini, unaambiwa hivi Ligi Kuu England imeshaheheni wanawake wa nguvu kabisa ambao wamekuwa na sapoti kubwa kwa waume zao katika kutimiza majukumu yao ya kuzitumikia klabu zao.

Hata hivyo, kwenye orodha ndefu kabisa ya wake, wachumba na mapatna wa wanasoka wa Ligi Kuu England, wapo wanaotajwa kuwa na mvuto mkubwa wakitajwa kuwa ni mademu bomba, pisi kali.

10) Edurne Garcia - mke wa David De Gea

Mrembo Edurne Garcia ni moja ya pisi kali inayomilikiwa na staa wa Ligi Kuu England. Edurne ni mwimbaji na mwigizaji wa Kihispaniola, ambaye yupo kwenye penzi zito na kipa wa Man United, De Gea - ambaye pia ni mmoja wa wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye Ligi Kuu England. Chochote anachofanya De Gea uwanjani, basi akirudi nyumbani anapata faraja kutoka kwa mrembo huyo matata kabisa.

9) Alysha Behague -mke wa Pierre-Emerick Aubameyang

Wanasema kwenye orodha ya warembo motomoto wa wake wa wanasoka wa Ligi Kuu England mmoja wao ni Alysha Behague, ambaye kipenzi cha straika wa Chelsea, Pierre-Emerick Aubameyang. Mrembo, Alysha alikutana na staa huyo wa Gabon miaka 10 iliyopita na wamekuwa wakionyesha maisha yao matamu kwenye mtandao wa Instagram. Mambo hayapo vizuri Chelsea na Auba anapata faraja kutoka kwa Alysha.

8) Izabel - mke wa Mateo Kovacic

Izabel ni mmoja wa wanawake warembo kabisa wake wa wanasoka kwenye Ligi Kuu England. Izabel ni maarufu sana huko kwao Croatia na kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo vinamfananisha na Shakira. Walifunga ndoa mwaka 2017 na mara kadhaa mrembo Izabel amekuwa akionekana jukwaani kwenye mechi anazocheza mume wake kwa ajili ya kwenda kumshangilia.

7) Leonita Lekaj - mke wa Granit Xhaka

Mrembo Leonita Lekaj ni mke wa kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka. Wawili hao walichumbiana Juni 2016 baada ya kuwa pamoja kwa miaka miwili na walifunga ndoa Julai 2017. Mrembo Leonita ni maarufu sana akiwa na wafuasi zaidi ya 185,000 kwenye Instagram. Xhaka anahusishwa na mpango wa kuondoka Arsenal na hilo likitokea, kama atatoka nje ya England, basi Ligi Kuu England itakuwa imepoteza pisi moja kali matata.

6) Sara Botello - mchumba wa Aymeric Laporte

Sara Botello akitokea tu hapo utaelewa kuna mwanamke amepita. Ni moja ya wanawake wa wanasoka wa Ligi Kuu England wenye mvuto mkubwa. Ndiye mpenzi wa beki wa Manchester City, Aymeric Laporte, ambao walikutana tangu kipindi beki huyo alikuwa akiichezea Bilbao. Kipindi hicho Sara, alikuwa akijihusisha na timu ya kikapu ya Bilbao. Baada ya kuanzisha uhusiano tu, Sara alihama Hispania na kumfuata mpenzi jijini Manchester.

5) Larissa Pereira - mke wa Roberto Firmino

Mrembo Larissa Pereira amekuwa mtu muhimu sana kwenye mafanikio ya mchezaji Roberto Firmino huko Liverpool. Bahati mbaya kwa msimu ujao, Larissa hataonekana kwenye mechi za Ligi Kuu England kwa sababu mume wake, Firmino atakuwa ameachana na Liverpool na kwenda kutafuta maisha kwingineko. Mrembo Larissa ni mwanamitindo maarufu mwenye wafuasi 157,000 kwenye mtandao wa Instagram.

4) Lorena Manas - mchumba wa Darwin Nunez

Mrembo Lorena Manas yupo kwenye penzi motomoto na straika wa Liverpool, Darmin Nunez. Wawili hao walitangaza kuzaliwa kwa wao wa kiume, Januari 2022. Lorena inaaminika ni rafiki mkubwa wa mke wa Lionel Messi, mrembo Antonella Roccuzzo. Mvuto wake unafanya Ligi Kuu England kuwa moja ya ligi yenye wachumba bomba kabisa wa wachezaji. Nunez bado anajitafuta kwenye maisha yake huko Anfield.

3) Muri Lopez Benitez - mchumba wa Lisandro Martinez

Mrembo wa Kiargentina, Muri Lopez Benitez amekuwa maarufu tangu mpenzi wake beki wa kati, Lisandro Martinez alipojiunga na Manchester United kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi. Muri amekuwa akiposti picha zake nyingi sana kwenye mtandao wa Instagram, lakini hakuna ubishi uwepo wake kwenye Ligi Kuu England unafanya jukwaa la Old Trafford kunoga nyakati ambazo anakwenda kumtazama mpenzi akikipiga.

2) Alisha Lehmann - mchumba wa Douglas Luiz

Mrembo Alisha Lehmann naye ni mwanasoka. Alitamba kwa miaka mitatu kwenye kikosi cha West Ham United kabla ya kusajiliw ana Aston Villa kwenye majira ya kiangazi ya mwaka 2021. Anatumikia pia timu ya taifa ya Uswisi. Umri wake ni miaka 23, lakini mrembo huyo ni mchumba wa mwanasoka Douglas Luiz. Luiz ni kiungo wa kati za Kibrazili, anayekipiga kwenye kikosi cha Aston Villa.

1) Ines Tomas - patna wa Bernardo Silva

Staa wa Manchester City, Bernardo Silva amepanga kufunga ndoa na mrembo Ines Tomaz huko kwao Ureno, Julai mwaka huu. Wakati mrembo Ines alipoonyesha kidole chake kikiwa na pete ya uchumba, Mei mwaka jana, aliweka wazi kwamba amekubali kuchumbiwa na Silva. Jambo hilo likafanya Ligi Kuu England kuwa na uhakika wa kuwa na shabiki mrembo kabisa kwenye majukwaa ya viwanja vyake kutokana na mrembo Ines kuwa mpenzi wa staa Silva.

Chanzo: Mwanaspoti