Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pique asema Arteta inafaa aje Barca

Mikel Arteta Speaks To Arsenal Player During Premier League Match Pique asema Arteta inafaa aje Barca

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa Barcelona, beki wa kati Gerard Pique amesema anaamini ipo siku kocha wa sasa wa Arsenal, Mikel Arteta atarudi kufanya kazi Nou Camp.

Arteta ni mchezaji wa zamani wa Barcelona na Pique anafichua kwamba kocha huyo wa Arsenal anaweza kufikiriwa na miamba hiyo ya Nou Camp wakati huu ambapo XaviHernandez anaelekea kung’atuka mwishoni mwa msimu huu.

“Kuinoa Barcelona unahitaji kuwa kocha wa aina fulani na ufahamu namna timu hiyo inavyocheza, hivyo machaguo yake yanakuwa ni machache sana sokoni,” alisema Pique.

“Bila shaka mmoja wao ni Guardiola, kwa sababu aliwahi kuwa Barcelona na ni mmoja wa makocha bora kwa sasa, sambamba na Arteta.

“Arteta naye ni mzuri pia. Anaifahamu Barcelona na alichezea Barcelona huko nyuma.”

Juu ya Guardiola kurejea Nou Camp, Pique alisema: “Hilo anapaswa kuulizwa yeye mwenyewe.

“Bado tunazungumza. Nina hakika watu wa Barcelona watapenda sana kumwona akirejea kundini.”

Arteta na kikosi chake cha Arsenal kwa sasa kinashika usukani wa Ligi Kuu England na kipo kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo kwenye droo iliyopangwa hivi karibuni watakipiga na miamba ya soka ya Ujerumani, Bayern Munich.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live