Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Manchester United, Gerard Pique amejikuta akidondoka kwenye jukwaa wakati alipokuwa akijaribu kusaini moja ya jezi za mashabiki huku akisilizia ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu yake.
Pique alikuwa nchini Mexico kuzindua michuano ya King League Americas, ambayo inahusisha timu za mpira wa miguu zenye wachezaji saba kila upande.
Baada ya kutoa uwasilishaji na kufungua rasmi michuano hiyo, Pique alisogea kwa mashabiki waliokuwa wameshika jezi wakitaka awasainie, wakati huo staa huyu alikuwa ameweka simu yake sikioni.
Lakini kabla hajamfikia shabiki husika alijikuta akitumbukia chini ya jukwaa na gazeti la Marca likaripoti alidondoka kwa uref mita mbili kwenda chini ingawa hakuumia.
Baada ya video hiyo kusambaa mashabiki walitoa mitazamo tofauti wengine walitania yalikuwa ni mazingaombwe na wengine wakasema alidondoka kwa hofu kwa sababu alikuwa akisiliza wimbo wa shakira kwenye simu yake.