Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pioli aisifu Milan na kauli yao ya kutokata tamaa

Pioli 2 E1580987307337 Stefano Pioli

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pioli aisifia kauli ya AC Milan ya kutosema haijshaisha mpaka iishe huku kauli hiyo ikiwa chachu ya ushindi kwenye mchezo wao wa jana walipokuwa ugenini dhidi ya Helles Verona huku dakika za lala salama bao la Sandro Tonali liliwapa mabingwa hao watetezi ushindi wa 2-1 kwenye Serie A.

Hayo ni maoni ya kocha mkuu Stefano Pioli, ambaye timu yake ilitangulia ndani ya dakika tisa kupata bao kupitia kwa mchezaji wake Miguel Veloso, lakini Verona walisawazisha punde baada ya shuti la Koray Gunter kutinga wavuni Matteo Gabbia.

Ushindi huo unawafanya Milan wapande hadi nafasi ya tatu kwenye Serie A, wakibakiza pointi tatu pekee nyuma ya viongozi Napoli huku wakipania kupata taji la pili mfululizo la ligi.

Pioli amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu, walianza vizuri kisha wakafanya makosa machache sana na wakaruhusu nafasi nyingi lakini kama kawaida timu iliweza kuvumilia na sifa zao zilifanya kushinda mchezo.

Alipoulizwa jinsi alivyokuwa na hisia chanya kuhusu kikosi chake kabla ya mechi nyingi, Pioli alijibu: “Tumefanikiwa kwa mara ya kwanza kushinda mechi tatu mfululizo kwenye michuano hii. “Tunakua, labda ningebadilisha kitu zaidi mwanzoni, lakini tunajua jinsi awamu hii ya msimu ilivyo muhimu, na kuanza na ushindi ndio njia bora ya kukabiliana na kipindi hiki.

Hakuishia hapo tuu, Pioli alisema kuwa kushinda michezo hiyo migumu kunamaanisha kuwa wanakua kiakili na katika ufahamu, ni kwamba hawakati tamaa. Huo ni ubora ambao timu yake wanao.

“Tunatumai kuwa na uwezo wa kurejesha nguvu na hata wachezaji wengine, kipindi muhimu cha ushindani kinatusubiri. Sisemi kwamba watakuwa na maamuzi kwa msimu mzima, lakini tumekaribia.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live