Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pilato fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya vilabu huyu hapa

Mustapha Ghorbal Pilato fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya vilabu huyu hapa

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi kutoka Algeria, Mustapha Ghorbal ameteuliwa kusimamia mchezo wa fainali ya kombe la Dunia la FIFA ngazi ya klabu kati ya Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid dhidi ya miamba ya Saudi Arabia, Al Hilal.

Mchezo huo utachezwa Februari 11, 2023 katika dimba la Prince Moulay Abdellah Mjini Rabat Moroco majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Real Madrid ilitinga fainali baada ya kuwalaza miamba ya Misri ????????, Al Ahly bao 4-1 huku Al Hilal ikifikia hatua hiyo kufuatia ushindi wa 3-2 dhidi ya miamba ya Brazil, Flamengo.

Al Ahly na Flamengo zitachuana kutafuta mshindi wa tatu Februari 11 katika dimba hilo majira ya saa 12:30 jioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live