Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mapema tu limewataja waamuzi wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali kati ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 30, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 3:00 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na CAF, mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Mohamed Omar, akisaidiwa na Mahmoud Ahmed Kamel Abouelregal na Ahmed Hossam Taha Ibrahim ambao wote ni kutoka Misri.
Mwamuzi wa akiba, atakuwa Mahmoud Nagy Ahmed Nagy Mosa ambaye naye ni raia wa Misri kama ilivyo kwa watu wa VAR, Mahmoud Ashor na Mahmoud Elbana.
Kamishna wa mchezo ni Amir Abdi Hassan kutoka Somalia, huku mtathmini wa waamuzi akiwa raia wa Angola, Inacio Manuel Candido. Gomezgani Zakazaka kutoka Malawi atakuwa ni mratibu mkuu wa mchezo, huku ofisa usalama akiwa Emmanuel Mutunami raia wa Zimbabwe.