Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pilato Simba vs Wydad huyu hapa

Pierre Ghislain Atcho.jpeg Pilato Simba vs Wydad huyu hapa

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC yenye pointi mbili kundi B itachezeshwa na Pierre Ghislain Atcho kutoka Gabon ambaye rekodi zinaonyesha amechezesha michezo 18 ya kimataifa na timu za nyumbani zilishinda tisa, sare nne na za ugenini zikishinda mara tano, huku akitoa jumla ya kadi za njano 77 na nyekundu moja.

Hesabu za Simba ni zilezile za kushinda mchezo ili pia kulipa kisasi kwani itafikisha pointi tano ikiiombea Jwaneng Galaxy ya Botswana itakayoifuata Mimosas nchini Ivory Coast ipoteze ili ikae nafasi ya pili.

Simba ina kumbukumbu ya kuifunga Wydad kwa bao 1-0 kwa Mkapa lililofungwa na Jean Baleke kwenye robo fainali ya michuano hiyo msimu uliopita, Aprili 22.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live