Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pigo la mwisho Sheik Jassim kwa Man United

Sheikh Jassim Wa Qatar Pigo la mwisho Sheik Jassim kwa Man United

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi Sheikh Jassim amejiondoa kwenye mchakato wa kuinunua Manchester United baada ya usiku wa Jumamosi kuwasemea mbovu wamiliki wa timu hiyo kwamba kiasi cha pesa wanachohitaji ili kuiuza timu ni cha kushangaza na cha ovyo sana.

Jassim ameondoka kwenye mchakato huo ikiwa ni baada ya miezi saba ya mazungumzo ambapo rasmi anakuwa ameiondoa ofa yake ya Pauni 5 milioni na amewaambia kabisa Glazer kwamba hana tena mpango wa kuinunua Man United.

Kuondoka kwa tajiri huyo kutoka Qatar kunampa nafasi Sir Jim Ratcliffe, ambaye anadaiwa kuhitaji kununua asilimia 25 tu za mashetani hao wekundu.

Sheikh Jassim amekuwa anaongoza kwenye mchakato huu wa kutaka kuinunua Man United tangu iwekwe sokoni Novemba mwaka jana.

Alijaribu kuvumilia licha ya kukerwa na mabosi wa Man United sambamba na wawakilishi wao waliokuwa wanasimamia mchakato huo Raine Group.

Matajiri hawa kutoka Qatar mpango wao ulikuwa ni kuinunua Man United mazima kutoka kwa Familia ya Glazer ambayo ilikuwa ikiimiliki klabu tangu mwaka 2005 ilipoinunua kwa Pauni 790 milioni, lakini walijaribu kuwasilisha ofa zaidi ya tano na zote zilikataliwa.

Ofa ya sita iliwasilishwa katika siku za hivi karibuni lakini pia ilikataliwa na Glazer wakaeleza kwamba wanataka kupewa Pauni 6 bilioni sambamba na kulipwa thamani ya hisa za timu hiyo kwenye soko la hisa la New York ambazo ni Pauni 2.7 bilioni ambapo jumla ingekuwa Pauni 7.7 bilioni, jambo ambalo limemkera Jassim na kuona hawezi tena kuendelea kutaka kuinunua klabu hiyo.

Jassim na washirika wake walikuwa wakiamini kwamba kiasi cha Pauni 5 bilioni walichoweka kilikuwa kinatosha kabisa kuinunua klabu hiyo na wangebakiwa na pesa ambazo wangetumia kukarabati miundo mbinu ya viwanja vya mazoezi, miradi mingine ya kijamii na kufanya usajili.

Lakini uvumilivu wao umefika kikomo na wameamua kuachana na mpango huo kwa sababu kila uchao familia ya Glazer imekuwa ikiwajia na bei mpya.

Vyanzo vya karibu na Sheikh Jassim vimekataa kutoa maoni yoyote juu ya hili lakini vilithibitisha kwamba tajiri huyo amejiondoa kwenye mchakato.

Kwa sasa Glazer wanaonekana kuwa na chaguo moja kati ya mawili ikiwa pamoja na kuuza baadhi ya hisa zao kwa Sir Jim Ratcliffe ama kuiondoa timu sokoni.

Hata hivyo, uamuzi wowote kati ya hayo, hautapunguza hasira za mashabiki wa Man United ambao wamechukizwa sana na kitendo cha Waarabu kujiondoa kwenye mchakato.

Mashabiki wana hasira kwa sababu walihitaji kuona timu hiyo ikinunuliwa jumla na sio kwa sehemu ya hisa kama anavyotaka kufanya Sir Jim.

Wengi wanaamini kwamba tatizo kubwa linalochangia anguko la timu yao linatoka kwa wamiliki. Man United kwa sasa inashika nafasi ya 10 kwenye EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live