Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha ya kusikitisha vichwani mwa wapenda soka

Gavi Picha Pablo Gavira 'Gavi'

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hiyo unayoiona hapo juu ni picha ya wiki yenye hisia mbaya zaidi kwa wapenda mpira wa miguu.

Pablo Gavira 'Gavi' anapata jeraha baya sana la Anterior Cruciate Ligament maarufu kama ACL, ambayo ni tishu inayounganisha mfupa wa paja na mguu.

Gavi atakaa nje miezi 9 kulingana na vipimo vya madaktari.

Taarifa mbali mbali zinaonesha kwamba FIFA watawalipa Barca kiasi cha Euro 20,548 katika siku zote ambazo Gavi atakosekana uwanjani ambapo kwa miezi 9 Barca wanaweza kujizolea karibia Euro milioni 5, kibongo bongo ni kama ni zaidi ya bilioni 13.

Kwa nini FIFA wanalipa vilabu hivi hasa wachezaji wao wanapoumia katika majukumu ya taifa? Sababu hata Real Madrid watapokea hela kutoka FIFA niliona baada ya jeraha la Eduardo Camavinga.

Mwezi Mei 2012, pale Budapest, Hungary kulikuwa na kongamano la FIFA na European Clubs Association (ECA) na katika kongamano hili walipitisha kitu kinaitwa Club Protection Programme (CPP) yaani Mpango wa Ulinzi wa Klabu.

CPP ni sera ya bima kwa wachezaji endapo mchezaji atapata majeraha akiwa analitumikia taifa lake, either ni kwenye mechi au kwenye mazoezi. Ili mradi tu, yawe ni mashindano ambayo yameandaliwa na kutambulika na FIFA. Na hii inamlenga timu za taifa za wanaume na wanawake.

So kwa kipindi chote ambacho mchezaji atakosekana uwanjani, FIFA watahusika isipokuwa tu swala la mshahara wa mchezaji.

Programu hii ilianza kazi kwenye michuano ya Euro 2012 pale Poland na Ukraine ambapo Hispania alishinda 4-0 dhidi ya Italia kwenye fainali kama mnakumbuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live