Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phoden apiga Hat Trick, Man City ikiichapa Brentford EPL

Phil Foden Hat Trick.jpeg Phoden apiga Hat Trick, Man City ikiichapa Brentford EPL

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Manchester City jana imetoka nyuma na kuwachapa wenyeji , Brentford City mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex.

Brentford walitangulia kwa bao la Neal Maupay dakika ya 21, kabla ya Phil Foden kufunga mfululizo dakika ya 45,53 na 70 hat trick ambayo imewarejesha nafasi ya pili mabingwa hao watetezi.

Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 49 katika mchezo wa 22 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili tu Liverpool ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Arsenal ni ya tatu ikiwa na pointi 49 pia za mechi 23.

Kwa upande wao Brentford City baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 22 za mechi 22 nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live