Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri bado aipasua Simba

Phiri Mbs.jpeg Moses Phiri

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba wanarudi mazoezini kwa sasa ili kujiandaa na michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 itakayoanza Alhamisi, huku ikielezwa mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Moses Phiri akiwavuruga na kuwagawa mabosi wa klabu hiyo kutokana na shinikizo la kutaka avunjiwe mkataba ili atimke zake.

Katikati ya wiki, Mwanaspoti lilipenyezewa taarifa kwamba Phiri ameamua kuandika barua ya kuomba kuondoka kla-buni hapo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, jambo linalomnyima furaha, japo mabosi wa klabu hiyo wanafanya siri kubwa, lakini taarifa za ndani zinasema mabosi hao wanahaha kumzuia.

Mbali na kumzuia, lakini taarifa zaidi zinasema kama msimamo wa Phiri utaendelea, basi watauvunja mkataba kwa masharti maalumu baada ya kushtukia kitu kwamba nyota huyo yupo kwenye rada za Yanga inayosaka straika kwa sasa kutokana na waliopo kikosini mwao kwa sasa kushindwa kuziba pengo la Fiston Mayele.

Mayele aliyemaliza kama kinara wa mabao wa klabu hiyo kwa misimu miwili mfululizo na kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita akilingana mabao 17 na nyota wa Simba, Saido Ntibazonkiza kwa sasa anakipiga Pyra-mids ya Misri, huku pengo la mshambuliaji likionekana kwa sasa licha ya Yanga kufunga mabao mengi kwenye mechi za ligi hiyo na ile ya kimataifa.

Habari kutoka Simba zinasema kuwa, mabosi wa klabu hiyo kwa sasa hawatulii kutokana na kutaka kumzuia mshambu-liaji huyo kuondoka na kuibukia Yanga kwa kuhofia lisiwatokee lile la Amissi Tambwe aliyeachwa kwenye dirisha dogo la msimu wa 2014-2015 na kutua Jangwani na kufanya makubwa wakiwaumiza Simba.

“Kwa sasa mabosi wanahaha kutuliza upepo wa Phiri, kwani amewachanganya na hasa baada ya kupata tetesi kwamba ameingia kwenye rada za Yanga. Wanaona wakimuachia kienyeji na kutua hapo watasumbuka kama ilivyokuwa kwa Tambwe aliyeibukia kwa watani na kufanya mambo makubwa tofauti na alivyochukuliwa akiwa Msimbazi,” kilisema chanzo hicho kilichoomba kuhifadhiwa jina.

“Leo (jana) jioni mabosi hao wanatarajiwa kukutana ili kujadili ishu hiyo ya Phiri, kwani mchezaji huyo kakomaa kutaka kuondoka, licha ya jana (juzi) kuwa benchi wakati Simba ikilazimishwa sare ya 2-2 na KMC kwenye Uwanja wa Azam Complex,” chanzo hicho kiliongeza.

Phiri, aliyemaliza msimu uliopita akiwa na mabao 10, hadi sasa amefunga mabao matatu katika Ligi Kuu, lakini akiwa ha-pati nafasi ya kutumika mara kwa mara tangu enzi za kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ raia wa Brazil aliyetimuliwa baada ya kichapo cha mabao 5-1 kutoka Yanga na hata sasa chini ya Abdelhak Benchikha.

Nyota huyo alisajiliwa na Simba msimu uliopita kutoka Zanaco baada ya mabosi wa Msimbazi kuwazidi wenzao wa Yanga waliokuwa wakimpigia hesabu na kumfuata hadi Zambia ili kumshawishi kutua Jangwani na alikuwa na wakati mzuri chini ya kocha Juma Mgunda akiibeba Simba Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na kwenye ligi kabla ya kuumia na kukaa nje kwa muda mrefu, hadi alipoingia Robertinho.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: