Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri awanyooshea kidole wachezaji wapya Simba

Phiri Kwa Mkapa.jpeg Moses Phiri

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba, Mzambia Moses Phiri amesema kila mchezaji mpya katika kikosi hicho anatakiwa kujitoa kulingana na majukumu ya nafasi yake ili kuongeza ubora wa timu kuwa tofauti na msimu uliopita.

Phiri alisema msimu uliopita Simba ilimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara na haikufanya vizuri Afrika ila msimu huu inatakiwa kuwa tofauti kwao kutokana na maingizo ya wachezaji wapya wenye uwezo kama kila mmoja atafanya kazi nzuri katika nafasi yake.

“Simba timu kubwa inahitaji ubora wa kila mchezaji ili kufanya vizuri kwa kushinda mechi mfululizo katika mashindano ya ndani pamoja na Ligi ya Afrika ili kupata mafanikio zaidi ya ilivyokuwa msimu uliyopita,” alisema Phiri na kuongeza;

“Ili wachezaji wapya tuliyoingia msimu huu thamani yetu kuonekana zaidi tunahitaji kupata mafanikio yaliyokuwa bora kwa kuchukua mataji ila tofauti na hivyo bado tutakuwa katika wakati mgumu,”

“Katika nyakati tofauti wachezaji tumekuwa tukifanya vikao vyetu wenyewe kuongea na kuhamasishana umuhimu wa kila mechi iliyokuwa mbele yetu kupambana hadi tone la mwisho ili kupata matokeo bora.

“Binafsi nahitaji kwanza kuona naisaidia timu kupata matokeo mazuri mfululizo kisha kufikia mafanikio ya kupata taji baada ya hapo nitaangalia mafanikio yangu binafsi kama mchezaji.

“Ambacho naamini kulingana na mashindano ya ndani nilivyo yaona naweza kuonyesha kiwango bora, kufunga mabao mengi zaidi ya wakati pamoja na kuisaidia timu kila ninapokuwa uwanjani.”

Simba msimu huu dirisha kubwa la usajili imesajili wachezaji nane, Phiri, Mohamed Ouattara, Habibu Kyombo, Dejan Georgijevic, Nassoro Kapama, Augustine Okrah, Nelson Okwa na Victor Akpan.

Phiri ndio mchezaji mpya aliyekuwa katika kiwango bora hadi sasa amefunga mabao matatu kwenye mechi nne za ligi na alifunga mabao mawili Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullet aliwafunga Zambia na hapa Tanzania mchezo wa marudiano.

Ouattara na Kyombo walikuwa wakicheza kikosi cha kwanza wakati kikosi hicho kipo chini ya kocha, Zoran Maki. Dejan katika mechi saba za kimashindano hadi sasa amefunga bao moja huku akiwa hana uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza wakati Akpan hajacheza mechi yoyote ya kimashindano.

Okrah ameifungia Simba bao moja kwenye mechi za kimashindano akiwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza wakati Okwa akiwa mchezaji wa kuingia kipindi cha pili ila amefunga bao moja katika mechi ya Simba Day dhidi ya St George kutokea Ethiopia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live