Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri avishwa mabomu kuwaua Singida Big Stars

Phiriiiiii.jpeg Moses Phiri

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri anatarajia kuongeza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo katika mchezo wa Leo dhidi ya Singida Big Stars.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni mkoani hapa ambapo mashabiki wengi wamejitokeza kuangalia burudani hiyo.

Kocha Juma Mgunda amemwanzisha Phiri mwenye mabao matano pamoja na Kibu Denis huku winga moja akianza Mzamiru Yassin

Kipa ataanza Beno Kakolanya huku mbavu ya kulia akicheza Shomary Kapombe na kushoto nahodha Mohammed Hussein 'Tshabalala.

Dimba la chini ameanza Jonas Mkude na dimba la juu ni Sadio Kanoute.

Beki wa kati Mgunda amemwanzisha Henock Inonga ambaye atashirikiana na Joash Onyango.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na timu zote kupata ushindi katika mchezo uliopita.

SBS waliwafunga Polisi Tanzania bao 1-0 huku Simba wakiwafunga Mtibwa Sugar 5-0.

Timu hizo zina pointi 17 zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Simba inashika nafasi ya 2 huku Singida ikishika nafasi ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live