Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri ambebesha zigo zito Chama

Phiri Goal Vs Agosto.jpeg Phiri ambebesha zigo zito Chama

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Moses Phiri amesema kuwa kiungo wao mshambuliaji, Clatous Chama ndiye atakayeamua kumpa ufungaji bora msimu huu.

Phiri hadi hivi sasa amefunga mabao 4 sawa na Sixtus Sabilo wa Mbeya City na Antony Mateo anayekipiga KMC, huku Reliants Lusajo wa Namungo FC akiongoza akipachika 5 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Staa huyo mpya wa Simba alijiunga na timu hiyo msimu huu kama mchezaji huru akitokea Zesco ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri alisema kuwa ngumu kwake kubeba ufungaji bora kama hatopata ushirikiano mzuri wa viungo wao wenye jukumu la kumchezesha.

Phiri alisema kuwa kati ya viungo ambao anaamini watampa ufungaji bora ni Chama mwenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho za kufunga mabao.

Aliongeza kuwa, kiungo huyo anarahisisha kufunga mabao kutokana na aina yake ya uchezaji, upigaji wa pasi na utulivu anapofika katika goli la wapinzani.

“Chama ndiye ninacheza naye pamoja pale mbele, yeye namba 10 na mimi 9, hivyo yeye ndiye atakayeamua hatima yangu ya ufungaji bora.

“Nimekuwa nikifurahia kucheza na Chama kutokana na umahiri wake mkubwa wa kupiga pasi akifika katika goli la wapinzani, na nafurahia zaidi utulivu alionao.

“Hivyo nishindwe mimi mwenyewe kutwaa ufungaji bora kama nikiendelea kucheza pamoja na Chama ambaye kwangu namuona ni namba kumi bora katika ligi hii,” alisema Phiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live