Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri akabidhiwa Tuzo yake Simba SC

Moses Phiri Tuzo Mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Zambia Moses Phiri amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi wa tisa wa klabu ya Simba siku ya leo pamoja na hundi ya milioni mbili katika ofisi za Emirates Alluminium.

Tuzo hiyo ambayo omekua ikitolewa kutokana na machaguo ya mashabiki wa klabu hiyo ambao hupiga kura kupitia tovuti ya klabu hiyo pamoja na kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Moses Phiri amekua na kiwango bora sana tangu aanze kupata nafasi ya kudumu klabuni hapo haswa ndani ya mwezi tisa, Mchezaji huyo amefanya vizuri klabuni hapo baada ya kufunga katika michezo saba iliyopita ya klabu hiyo.

Moses Phiri ameibuka na kufanya vizuri klabuni ndani ya Simba licha ya taarifa zilizotoka kua hakua akihitajika na kocha aliepita klabuni hapo bwana Zoran Maki alietimkia nchini Misri.

Mshambuliaji huyo akiwa pamoja na afisa mahusiano wa kampuni ya Emirates Aluminium wanaodhamini tuzo hizo walikutana leo hii ni staa huyo wa kimataifa wa Zambia kukabidhiwa tuzo yake na kiwango cha pesa baada ya kazi kubwa aliyoifanya ndani ya mwezi wa tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live