Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri aibua matumaini mapyww Simba Sc

MOSES PHIRI SHUKURANI 1.png Phiri aibua matumaini mapyww Simba Sc

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupata majeraha ya mguu wa kulia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kiungo mshambuliaji wa Simba Moses Phiri amefanyiwa vipimo ambapo majibu ya wali ya vipimo hivyo yamethibitisha straika huyo kutopata majeraha makubwa kwenye mguu huo huku akitarajiwa muda wowote kurejea uwanjani.

Phiri alilazimika kutolewa dakika ya 80 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikichukuliwa na Kibu Dennis ambapo baada ya mchezo huo taarifa za majeraha yake ziliibuka kuwa huenda akakaa nje kwa kipindi kirefu akiuguza jeraha lake.

Akizungumza, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alifunguka: “Phiri amefanyiwa vipimo viwili ili kuangalia ukubwa wa jeraha lake na habari njema ni kwamba vipimo vya awali vimeonyesha kuwa hajavunjika mguu hivyo tunaendelea kusubiri ripoti kamili ya madaktari kuona itamchukua muda gani hadi kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

“Nitoe rai kwa wachezaji wote kwenye ligi yetu kuendelea kusimamia mchezo wa kiungwana kwani mpira ndiyo ajira yao hivyo kuchezeana rafu ambazo zinahatarisha maisha ya mchezaji mwenzio siyo kitendo cha uungwana na si cha kiuanamichezo hivyo wanatakiwa kuwa mabalozi wa kupigania mchezo wa kiungwana na siyo kuwa sehemu ya wenzao kukatisha ndoto zao,” alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live