Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri achana mkataba Simba

Phirii Goal.jpeg Phiri achana mkataba Simba

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Simba Moses Phiri ameandika barua ya kuvunja mkataba wake jambo ambalo linadaiwa kubarikiwa na mabosi hao, hivyo muda wowote huenda wakatangaza kuachana naye.

“Siku mbili hizi tutakuwa na kikao juu ya mustakabali wa haya yote ikiwamo usajili. Ishu ya Phiri ni kweli ipo maana naye ameingia kwenye mfumo ule ule wa wenzake, hivyo kwake lolote linaweza kutokea kwasasa.”

Wakati wa mechi ya Wydad, Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha alimwondoa Phiri na Jimson Mwanuke kwenye kikosi ambacho kilicheza mechi hiyo baada ya nyota idadi kuzidi.

Idadi iliyokuwa inatakiwa kwa mujibu wa kanuni za CAF ni wachezaji 20 lakini Simba ilikuwa nao 22, hivyo ilimzalimu kocha kuwaondoa wawili hao kitendo ambacho pia kinadaiwa kutafsiriwa vibaya na mshambuliaji huyo raia wa Zambia na kuchukuwa uamuzi wa kuomba kuvunja mkataba.

Benchikha alisema hamna mkubwa kuliko klabu.

Chanzo: Mwanaspoti