Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phil Foden avunja rekodi ya Lionel Messi

Phil Foden Nn Haaland akimpongeza Foden baada ya kufunga magoli matatu

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Phil foden amefanikiwa kuvunja rekodi ya Lionel Messi baada ya kufunga katika mchezo wa derby ya Manchester leo mapema katika dimba la Etihad.

Phil Foden anakua mchezaji mdogo zaidi wa kwanza kufunga magoli 50 kwenye timu anayofundisha Pep Guardiola baada ya kufunga leo akiwa na umri wa miaka 22 na siku 127 huku Lionel Messi yeye alifikisha magoli hayo akiwa na miaka 22 na siku 164 wakati huo akiwa chini ya Pep katika klabu ya Fc Barcelona.

Hivo kinda huyo wa kiingereza anakua ndio kinara kwa sasa katika vijana ambao wamewahi kufunga mabao 50 chini ya mwalimu huyo, kitu chqa kukumbuka pia ni kua Messi akishaichezea Barcelona kwa misimu minne kabla Pep hajachukua timu mwaka 2008/09 huku Foden yeye akicheza chini ya kocha huyo tu.

Phil Foden toka alipopewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na mwalimu Pep Guardiola amekua na kiwango bora sana na kukiendeleza kiwango hicho huku akifanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwenye ligi hiyo mara mbili mfululizo.

Kiungo huyo wa kiingereza amefanikiwa kutakata leo katika mchezo wa Deby baada ya kufunga magoli matatu sawa na mshambuliaji matata wa klabu hiyo Earling Haaland.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live