Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Petro de Luanda yaikomalia Mazembe nyumbani

Mazembe Vs Petro Petro de Luanda yaikomalia Mazembe nyumbani

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Petro de Luanda ya Angola leo imeitibulia rekodi TP Mazembe baada ya kutoa suluhu katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa mjini Lubumbashi, DR Congo.

Katika mchezo huo ambao Mazembe ilikuwa nyumbani na kulazimisha sare, timu hiyo ilimiliki mpira kwa asilimia 60 dhidi ya 40 za Petro, lakini hadi mwisho hakukuwa na mbabe.

Mazembe tangu katika hatua ya makundi haijapoteza mchezo wowote wa nyumbani na hii inakuwa ya kwanza dhidi ya Waangola msimu huu kutoka suluhu, huku Petro ikiendeleza rekodi ya kutopoteza kufikia mechi saba mfululizo.

Desemba 2, mwaka jana iliifunga Mamelodi Sundowns kwa bao 1-0 kisha ikaifunga FC Nouadhibou ya Mauritania kwa mabao 2-0 na Pyramids 3-0.

Mbali na Mazembe, pia Waangola hao wanaendeleza rekodi ya kutoruhusu bao ukiwa mchezo wa saba baada ya ile sita ya hatua ya makundi.

Mechi ya pili kati ya timu hizo itapigwa Aprili 6 katika Uwanja wa Estadio 11 de Novembro mjini Luanda, Angola na Mazembe ikiwa ugenini itakuwa na kibarua cha kupigania hatima yake ya kutinga nusu fainali baada ya miaka sita kupita. Mara ya mwisho kucheza hatua hiyo ilikuwa msimu wa 2018/2019.

Chanzo: Mwanaspoti