Shirikisho la Soka la nchini Angola lilitoa andiko rasmi la kuifungia Klabu ya Petro de Luanda kutojiusisha na masuala ya soka kwa miaka miwili.
Andiko hilo lilitolewa siku kadhaa nyuma baada ya tarehe ya droo ya African Football League kutangazwa shirikisho likiaminI De Luanda ingeondolewa pia katika michuano hyo lakini bado watashiriki.
Rais wa Klabu ya Luanda, Tomás Faria kwenye mkutano na waandishi wa habari amelishtumu shirikisho hilo kuwa ni la mchongo.
Rais huyo amesema ukiangalia andiko na sababu za kufungiwa kwao utagundua kuna mtu nyuma ya hili na lengo ni kuichafua klabu hii mbele ya uso wa Soka la Afrika.
Rais huyo amehtimisha kwa kusema; "Hatujafungiwa wala kusimamishwa, na hatutalipa faini wala hela kwa mtu yoyote na timu itashiriki ligi kuu kama kawaida," amesema Faria.
kama hali itaendelea hivi basi ili suala tutalipeleka ngazi za juu zaidi .