Klabu ya Petro Atletico imeachana na kiungo wake, kiungo wa zamani wa Yanga Sc, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo almaarufu Carlinhos sio kwa sababu ya kiwango chake bali kutokana na sababu za nje ya uwanja.
Duru mbalimbali nchini Angola zinaeleza kuwa, Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila mambo ya nje ya uwanja ndiyo yanayofanya asiwe nyota mkubwa Afrika.
Klabu ya Cape Town City ya nchini Afrika Kusini imefikia makubaliano ya kumsajili Carlinhos kutoka Petro De Atletico ya Angola.
Carlinhos (29) raia wa Angola anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye chaguo la kuongezeka na tayari amefanyiwa vipimo vya afya.
Carlinhos Carmo aliondoka Young Africans SC kwa makubaliano ya pande mbili kwa sababu za nje ya uwanja pia.