Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Peter Schmeichel: Onana haaminiki hata na Wachezaji langoni

Peter Schmeichel Speak.jpeg Peter Schmeichel akimzungumzia Onana

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Peter Schmeichel anaamini wachezaji wenzake Andre Onana wameanza kupoteza imani na kipa huyo wa Manchester United kwamba haaminiki tena baada ya kufanya kosa jingine dhidi ya Brentford.

Baada ya kukiri kwamba Onana hakuwa amejiandaa kwenye lile bao la kwanza la Brentford, kipa huyo wa zamani Schmeichel alisema: “Nayawazia sana haya makosa ya Onana ni presha. Nilizungumza naye baada ya mechi ya Bayern Munich. Nilizungumza naye baada ya mechi ya Galatasaray na alionekana kuvunjika moyo kutokana na makosa ambayo amekuwa akifanya.

“Nilimwambia vile mambo yanavyokuwa unapokuwa mchezaji wa Manchester United. Unapofanya kosa unapaswa kuliweka kando na kufikiria mambo ya mechi inayofuata. Kuna makosa yanayoonekana na kuna yale ambayo hayaonekani na wote.

“Lakini, unapotoka kwenye mechi unapaswa ufanye uchambuzi mwenyewe wa kile kilichotokea na kufikiria mchezo mpya. Usipofanya hivyo, utafanya makosa mengine katika mchezo unaofuata. Na sasa amemvuruga kila mtu kwenye timu. Hawamwamini kabisa, hii siyo nzuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live